ABNA- Watu 19 wauliwa na wengine 72 kujeruhiwa katika milipuko ya mabomu dhidi ya misikiti mitatu ya Kishia mjini Bagdhad.
Polisi wa Iraq wamesema, milipuko hiyo ilitokea baada ya magari yaliyokuwa yametegwa mabomu na kulipuka karibu na misikiti hiyo na kusababisha vifo vya waumini hao wa Kishia. Mpaka sasa hakuna kundi lolote ambalo limekiri kuhusi na shambulizi hilo.